RC Makonda aongeza nguvu kazi ya Madaktari zoezi la upimaji afya

https://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/rc-makonda-aongeza-nguvu-kazi-ya.html
Kutokana na Idadi kubwa ya Wananchi waliojitokeza kwenye Zoezi Upimaji na Matibabu Bure ndani ya Meli ya Jeshi la Jamuhuri ya China, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. PAUL MAKONDA ameongeza nguvu kazi ya Madaktari Bingwa kwaajili ya kuhakikisha kila aliepatiwa namba anahudumiwa.
Katika kikao Kati ya RC MAKONDA na Kamanda wa Jeshi la Jamuhuri ya China, Madaktari wa China wameridhia kuongeza muda wa kutoa huduma kwa kupunguza muda wa Mapumziko kutoka masaa Matatu hadi lisaa limoja pamoja na kutoa matibabu usiku na Mchana.

Aidha RC MAKONDA amesema kuwa wameongeza Vituo Vitatu vya kutolea huduma ambapo wapo watakaotibiwa eneo linalotumika kugawa namba (central), pembezoni mwa Meli na ndani ya Meli kwa wale wagonjwa weliozidiwa Sana.
Aidha RC MAKONDA amesema hadi sasa zaidi ya Wagonjwa 17 wamefanyiwa Upasuaji Mkubwa Bure kitendo ambacho kimesaidia kupunguza gharama za matibabu ikiwemo kusafirisha wagonjwa Nje ya Nchi.