Mratibu wa Simba aikaribisha Yanga mezani

Zile tetesi za mchezaji wa Klabu ya Simba Mo Ibrahim kutajwa sana upande wa pili klabu ya Yanga huenda JAMBO hilo likawezekana mara baada ya Maratibu wa Klabu ya Simba Abbas Suleiman kufunguka kuwa licha ya Mo Ibrahim kuwa bado ni mchezaji wa Simba mwenye mkataba ila kama mambo yatafuata Utaratibu na Uongozi pamoja na benchi la Ufundi likawa tayari kumwachia basi huenda mchezaji huyo akatua Jangwani.
Image result for mo ibrahim simba
Akiongea na Kituo cha radio cha Dream Fm cha Jijini Mbeya Abbas Suleiman   amesema

Of course tetesi zipo lakini sisi kama taasisi tumejipangia utaratibu wa kufanya kazi hatufanyii kazi tetesi, tukisema tufanyie kazi tetesi wakati Mo ni mchezaji halali wa Simba na tunajua mkataba wake unafahamika lakini Yanga kama wanamwitaji Mo zipo taratibu ambazo wanaweza wakazifata wakaweka mezani viongozi wa Simba ni wasikivu wanaweza wakaangalia umuhimu wa Mo wanaweza wakaangalia kiwango cha Mo wakafikia Makubaliano.


Abbas Suleiman amesema pia Mo anaamani ndani ya Simba na Anafuraha ila kwakuwa mpira wa nchi hii umetoka kwenye professionalism umeingia kwenye siasa kwakuwa tu katiba ya nchi unaruhusu watu kuongea basi wanawaacha watu waongee. 

Related

michezo 315533703571186193

Post a Comment

emo-but-icon

item