Tausi Entertainment yashauri Vijana kufanya kazi zenye ubora badala ya kukimbilia ustaa

https://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/tausi-entertainment-yashauri-vijana.html
TAUSI Entertainments &
Talents ni miongoni mwa Kampuni ya Kitanzania iliyoanzishwa Mei, 2016 huko Zanzibar ikiwa na lengo la
kusaidia Vijana wa Kitanzania katika kukuza tasnia ya muziki.
Akizungumza na Raia Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tausi
Entertainment & Talent , Tausi Omary Mohamed , amesema lengo la kuanzisha
kampuni hiyo, kumetokana na kutaka
kusaidia tasnia ya muziki kwa wale watakao kuwa na uhitaji na wenye uwezo ambao kampuni yake itakuwatayari
kufanya nao kazi.
![]() |
Mkurugenzi Tausi Omary Mohamed |
Aidha, Tausi, amesema kuwa kampuni hiyo ilianzishwa ikiwa na wasanii watatu,
hadi kufikia Julai mwaka 2017, ilibakiwa na msanii mmoja Chidy Grenade , hivyo
aliamua kumsaninisha mwengine Oktoba , 2017 ambaye ni Sharara Tz kutoka Dar es Salaam.
Miongoni mwa wasanii maarufu waliokuwa wakimilikiwa
na Tausi Entertainment & Talent ni
pamoja na Sultan King pamoja na Berry
Black ambapo kwa sasa hawako tena kwenye
kampuni hiyo.

Mbali na kujihusisha na maswala ya
muziki lakini kampuni hiyo imeanzisha program ya Tausi Entertanment Search
ikiwa na lengo la kusaka vipaji kama vile vichekesho, uimbaji pamoja na ku
dansi (shake).
Programu hiyo ya Talent Search
inafanyika mara moja kila mwaka huku pambano jengine likitarajiwa kufanyika
mwakani Agosti 2018 Zanzibar.
“ Mimi sikuanzisha kampuni kwa ajili
ya kushindana, najua zipo kampuni nyingi zinazosimamia wasanii, lakini lengo ni
kusaidia Vijana hususani Zanzibar katika kuwapatia ajira ,na kufikia malengo
yangu, hata kama zitaongezeka siku hadi siku sina shida maana kila mtu ana
malengo yake.”Amesema Tausi

Huyu ni mwanamke aliyethubutu kutoa alichonacho na
kuona wengine wakinufaika nacho, lakini aliendelea kushikilia msimamo wake wa
kuhamisha Tausi Talent Search Dar es Salaam baada ya kukamilisha mipango yake.
Miongoni mwa mafanikio aliyoyapata ni pamoja na kuwa
na Mnyororo mkubwa wa watu wanaosaidiana katika kufikia malengo yake kama vile
mitandao ikiwamo TV, Magazine na Redio
Kuhusu kuchukua wasanii mkubwa na wanae, amesema
lengo lake ni kutaka kushirikiana nae pale atakapo wahitaji wasanii hao kufanya
nao kazi na wala sio kuwaiba.
Hivi sasa yupo katika mpango wa kuhakikisha anakuwa
na Vijana wenye vipaji wengi watakao weza kuutangaza vema muziki wa Tanzania
kimataifa kama ilivyo kwa wasanii wengine kama viele Ali Kiba na Diamond
wanaoonekana kuliteka soko la Afrika Mashariki kwa sasa.
Aidha, Mkurugenzi Tausi amesema kuwa Vijana wanaochipukia wasiwe na haraka ya kuwa star
wanatakiwa wafanye kazi zenye ubora na
wawe na nidhamu na subira katika kufikia malengo.