Zahera akunwa na kiwango cha Ajibu na kusema atakuwa tishio zaidi















KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera, amekiri kuwa kwa sasa mshambuliaji wake, Ibrahim Ajibu amekuwa akiibeba timu hiyo, lakini amepanga kumbadili kwa kumpa makali zaidi.

mshambuliaji wa yanga ibrahim ajibu picha na mtandao
Zahera, amesema nyota huyo ana uwezo mkubwa na anaweza akacheza kwa kiwango cha juu zaidi kama atabadilika kidogo.

“Ni mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa sana kumuona hapa Tanzania..., ana kila kitu ambacho mchezaji anapaswa kuwa nacho, mapungufu aliyonayo ndio ninayoyafanyia kazi na kama atabadilika atakuwa na moto mkali uwanjani,” alisema Zahera.

“Ni mchezaji mzuri na kwa sasa amekuwa na mchango mkubwa kwa timu, anajua nini cha kufanya akiwa na mpira,” aliongeza kusema.

Mpaka sasa Ajibu ameifungia timu yake mabao matatu na kutengeneza ‘assists’ nane kwenye mechi saba walizocheza mpaka sasa.

Mshambuliaji huyo amekuwa na kasi na kiwango cha juu msimu huu ambapo kocha Zahera, amesema kiwango hicho kinatokana na Ajibu kubadilika na kujituma zaidi mazoezini na kufuata maelekezo yake.

Mashabiki wa timu hiyo watamshuhudia tena Ajibu uwanjani kesho wakati kikosi hicho cha Zahera kitakapowakabili KMC kwenye mchezo wao wa nane wa Ligi Kuu msimu huu.

Michezo mingine ya ligi hiyo kesho itashuhudiwa pia Mbeya City ikiwakaribisha Mwadui, Ndanda ikiwaalika Biashara United wakati Mbao FC itakuwa nyumbani Mwanza kucheza na Lipuli huku Stand United ikicheza na Mtibwa Sugar.

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

item