UNESCO yawataka Waandishi wa Habari nchini kutoa taarifa za maendeleo
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/10/unesco-yawataka-waandishi-wa-habari.html

SHIRIKA la la Elimu Duniani kupitia makao ya Tanzania, limewataka Waandishi wa Habari kujikita zaidi kwenye Habari za maendeleo wakati wa kuelekea malengo endelevu ya Maendeleo ya 2030.
Hayo yamesemwa Leo na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa UNESCO Tanzania, Christiana Musaroche, amesema taaluma ya Habari ni taaluma ngumu yenye wajibu wa kutoa Habari za maendeleo na kuamsha hari ya utendaji kuongezeka kwa kile wanachokiandika.
Katika Semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi uliokuwa Wizara ya Elimu zamani Jijini Dar es Salaam, amewataka waandishi kuendana na Sera ya mpango wa Maendeleo endelevu ( SDG,s) ambao unataka hadi kufikia 2030 watu wote waishi katika maisha bora na kuondokana na umasikini.
Aidha, Musaroche amesema kuna haja kubwa yakafanyika maboresho katika Sekta ya Habari na vyombo vyote kwa ujumla ili kuwapa nafasi na haki za upatikanaji wa Habari kwa Waandishi waliopo nchini.
" Waandishi wa Habari wanajukumu kubwa la kuelimisha Jamii hususani katika kutoa Habari zenye viashira vya maendeleo lakini yote watafanikiwa endapo watazingatia misingi ya taaluma yao" Amesema Musaroche.
Amesema pamoja na changamoto zinazoikabili sekta ya Habari hapa nchini , bado wanapaswa kujitafakari na kuwa wabunifu kwani kwenye changamoto ndipo fursa hutokea. Licha ya kueleza hayo, amesema bado Waandishi wana nafasi kubwa ya kuelimisha umma kwahiyo midahalo izidi kufanyika na kuzidi kutoa elimu ili jamii itambue unuhimu wa Habari katika kufikia malengo hususani katika jamii zilizofungwa ( Closed Societies).
Aidha ameziomba mamlaka husika zitoe ushirikiano kwa waandishi wa Habari ili kujua wapi walipotoka, walipo na wanapokwenda katika Sera za uwezeshwaji wa mpango wa maendeleo endelevu.
Amesema Haki za upatikanaji wa taarifa juu ya mpango wa maendeleo endelevu inatakiwa taarifa zake ziwe wazi ili jamii ifahamu mpango mbali mbali inayoratibiwa inafanyiwa kazi kwa wakati na malengo mahususi.
Katika Hatua nyingine, Mtoaji wa maada katika semina hiyo ambaye ni mhadhili msaidizi kutoka chuo kikuu cha Tumaini Tawi la Mkoa wa Dar es salaam, Mary Kafyome, amesema kuwa nchi nyingi kama Brazil, Mexico, Cameroon zilifanikiwa kutoka na na haki za kupata Taarifa , hivyo Waandishi wa Tanzania wanatakiwa kuiga mifano hiyo ili Taifa lipige hatua.
Amesema kuwa, haki ya upatikanaji wa Habari ni nguzo muhimu ya kutanua wigo na kufanya usawa wa maendeleo kati ya jamii zilizo wazi na zilizofungwa.
Aidha amesetaja changamoto kadhaa ambazo zilikadiliwa na waandishi huku akitoa rai na angalizo jinsi ya kukabiliana na kufanya Taifa la Tanzania linaingia katika rekodi ya kuaga umasikini.
" Nimefanya tafiti zangu nimegundua yapo matabaka katika jamii zetu, lakini njia pekee itakayowezesha kufanya uwiano sawa ni kupatikana kwa haki za taarifa katika jamii" Amesema Kafyome.
Amesema hadi kufikia mwaka 2030 Taifa linatakiwa kuondokana na umasikini, hivyo kuna kila sababu za Waandishi wa Habari kutumia kalamu zao kwa makini kuonyesha jamii jinsi gani wanahitaji kuwajibika na vuongozi kuona umuhimu wa kusaidia tasnia ya Habari ifikie malengo.
Naye Afisa programu katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Lusajo Mwaiterike, amesema lengo lao ni kufikia vyombo vyote vya Habari hapa nchini ili kuamsha hali ya maendeleo kupitia Waandishi wa Habari waliopo Vijijini.
Pia amesema semina wanazozifanya zinalenga kuinua uwajibikaji kwa jamii katika kufikia mpango wa maendeleo endelevu ( Sustainable Development Goals) .
Katika semina hiyo, ziliibuliwa hoja mbali mbali zinazopelekea kutokupatika kwa taarifa za Habari zenye kulenga maendeleo kwa jamii .
Miongoni Mwa changamoto zilizoibuliwa katika semina kati ya UNESCO pamoja na Waandishi wa Habari ni pamoja na Sheria kandamizi katika tasnia, Ukosefu wa Rasilimali fedha, Sera za vyombo vya Habari husika, kutokuzingatia maadili ya uandishi wa Habari pamoja na Rushwa kati ya mwandishi na mtoaji taarifa.


