Mkurugenzi Ilala akoshwa na ubunifu wa kiutendaji wa Shirika la Apps & Girls katika ufundishaji wa Elimu ya TEHAMA

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/10/mkurugenzi-ilala-akoshwa-na-ubunifu-wa.html
MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri, amelipongeza Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na ufundishaji wa Elimu ya TEHAMA, hapa nchini lijulikanalo kwa jina la APPS AND GIRLS , kwa kazi nzuri ya ubunifu na ualedi katika kumuwezesha Mtoto wa kike kujikomboa kiuchumi.
Hayo ameyazungumza leo na Waandishi wa kwenye Shule ya Sekondari Kisutu ,ambapo Shirika hilo lilikuwa likizindua Siku ya Wiki ya Mwafrika kitaalamu hujulikana kama “Week Code Afrika” yenye kauli mbiu isemayo “Codeing is a New Language, Every Child Deserves to be Fluent”.
Mara baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Jumanne Shauri, amewataka Wanafunzi hao waliopatiwa Masomo ya elimu ya TEHAMA kuhakikisha kwamba Elimu hiyo wanaiwekea mkazo na kuipa kipaumbe ili kujikomboa kwa kubuni Application mbali mbali zitakazo wafanya waweze kujipatia kipato kupitia kwa Wasomaji pamoja na wawekezaji.
Aidha, amesema Matajiri wote wakubwa Duniani, wamepata pesa kwa ajili ya elimu ya TEHAMA iliyowasababisha kuweza utatua changamoto za kijamii katika masuala mazima ya uchumi.
Amesema kwamba somo la I.T ndilo lililompelekea hadi anakuwa katika nyadhifa tofauti tofauti ikiwamo ya Ukurugenzi hii yote ni kutokana na kuijua kiundani elimu ya TEHAMA na kupenda kujifunza kila siku. “Kipindi cha nyuma kabla ya utandawazi kuenea katika Taifa letu, watu wa I.T walikuwa wachache sana, hivyo tukajikuta tupo wachache lakini mimi nilikuwa mmojawapo wa waanzilishi wa kutenegeneza applications mbali mbali ikiwamo ya Tanzania Beyond Tommorow, hivyo kwa sasa Teknolojia hii ni pana jikiteni katika I.T , isomeni sana itawasaidia mbeleni kwani soko la ajira ni gumu lakini ukiwa na taaluma yako ya I.T utafurahia maisha na utaweza kufikia ndoto zako na kuwa tajiri ”Amesema Mkurugenzi Jumanne Shaibu
Mkurugenzi huyo ameenda mbali zaidi kwa kutolea mfano Nchi ya Ujerumani huku akisema kwamba wenzetu kule elimu ya TEHAMA inayotolewa nchini kwetu kwa Shule za Sekondari wao wanaitoa katika Shule za Msingi hii inatokana na kwamba wenzetu wamepiga hatua sana katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Hta hivyo, Mkurugenzi huyo katika kuona Elimu ya TEHAMA inakuwa na Tija katika Manispaa yake ya Ilala, amesema mwakani atajitahidi kuingiza katika bajeti ili kila Shule iliyopo Mnaispaa ya Ilala yenye Umeme inapatiwa Kompyuta 5 katika kukuza elimu ya I.T Shuleni.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mahusiano ya Umma Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, amewataka Watoto wakike hao waliyopata nafasi ya kusoma elimu ya TEHAMA watumie fursa hiyo kwa asilimia 100 kwani ndio njia pekee ya kuwawezesha kiuchumi na kumlinda motto wa kike dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia na kuona Wanawake wakiwezeshwa wanaweza.
Amewataka wale wote waliohudhuria elimu hiyo, waifikishe kwa wengine ili kufanya Teknolojia ya Sayansi kuzidi kushika kasi ndani ya Manispaa na Taifa kwa ujumla hususani katika Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati.
“Nimefurahishwa sana na Elimu hii, kwangu imekuwa kivutio kikubwa, hii inaonyesha ni jinsi gani Mtoto wa Kike anavyopewa kipaumbele , tumeshuhuida mabadiliko makubwa sana ya kiutawala hapa nchini kwa kumpata Mkamu wa Rais Mwanamke hii inaonyesha mbadiliko makubwa sna na nyinyi igeni mfano huo kuchochea mabadiliko chanya katika jamii na kuleta usawa katika maendeleo hivyo siku ya leo nimefarijika sana na itaongeza kitu katika I.T” Amesema Tabu Shaibu.
Katika hatua nyingine, Mwanzilishi wa Shirika la Apps & Girls, Carolyine Ekyavisuma, amesema Shirika hilo lilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2013, likiwa na Klabu moja lakini kwa sasa wana Klaabu 24 katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo jumla ya Klabu 4 za Shule Binafsi na Klabu 20 Shule za Seikali.
Amesema kwa sasa wapo mbioni kufanya Kongamano la kutoa elimu ya Ujasiriamali kupitia maarifa ya Kompyuta, ambapo yatafanyika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Posta November 9-10, 2018.
Aidha, amesema mpaka sasa wamewafundisha Waalimu 270, ambapo Mkoa wa Dar Waalimu 52, Kisarawe 43, Zanzibar 95 na Dododma 80.
Amesma leo walikuwa wana adhimisha Afrika Code Week, ambapo zaidi ya nchi 35 zinaanda matukio kama haya kwa Wanafunzi ambao hawakupata mafunzo ya TEHAMA.
Amesema kesho watakuwa Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuendelea na Programu zao amabapo watakapo rudi Mkoa wa Dar watafikia katika Shule mbili za Sekondari ikiwamo Jamhuri na Shule ya Sekondari Dar es Salaam.
Kwa upande wa Mwanafunzi Noela Christian Ngowi ambaye yupo kidato cha tano Shule ya Sekondari Kisutu, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala katika kuhuhudhuria uzinduzi wa program yao huku akisema kitendo hicho kimewapa moyo na ujasiri mkubwa wa kufanya mambo makubwa kwa kujiamini.
Pia mwanafunzi huyo, amemuomba Mkurugenzi huyo wapatiwe Semina elekezi za mara kwa mara angalau mara moja kwa mwezi zitakazo lenaga kumuwezesha Mtoto wa Kike Shuleni kujitambua lakini Afisa habari amelichkua hilo kwa niaba ya mkurugenzi wa Manispaa na kusema atalifanyia kazi kwa kushirikiana na watu wa Ustai wa Jamii.
Naye Martida Moses Mashauri, amesema ushauri wa Mkurugenzi wataufanyia kazi huku akimuomba Mkurugenzi huyo kuwawekea Kompyuta shule zao na mkurugenzi baada ya hapo alilipokea na kusema atalifanyia kazi.
Ikumbukwe katika uzinduzi huo wa Code Week Afrika, Shule za Sekondari mbili zikiwamo Gerezani na Kisutu ziliungana kwa pamoja.