Afisa Habari Manispaa ya Ilala awataka Watendaji kuiga mfano wa Diwani Kata ya Kisukuru







Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasilianao na Mahusiano kwa Umma, Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, amewataka watendaji waache kujibwetaka badala yake waige mfano wa Diwani wa Kata ya Kisukuru, Mh: J oseph Saenda katika kuleta maendeleo.

Hayo ameyasema leo mara baada ya kutembelea katika kata hiyo na kuona jinsi Diwani huyo alivyo bega kwa began a wananchi wake katika kurekebisha kipande cha bara bara ya Maji Chumvi Bonyokwa chenye urefu wa Kilomita za mraba 2.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Afisa habari huyo, amempongeza Diwani huyo kwa kazi nzuri ya kuunganisha nguvu za Wananchi katika kuchagiza maendeleo katika Kata yake.
Amesema mfano huo uigwe na Watendaji wengine kama nia mbadala ya kutataua matatizo ya Wananchi badala ya kusubiria kila kitu Serikali ilete.

Amesema ni mara chache sana Katika Mkoa wa Dar es Salaaam, Wananchi kuacha shughuli zao kujiunga na shughuli za kijamii , hivyo kitendo alichokifanya diwani huyo kila mtendaji au Diwani akikifanya kitapelekea kutatua maeneo mengine kero ndogo ndogo.

“Katika maendeleo lazima nguvu zote zitumke, Serikali pamoja na Wananchi wakishirikiana kwa pamoja hizi changamoto za kusubiria bajeti ya Serikali zitapungua, Serikali haiwezi kutatua kero zote lazima nyingine viongozi mjiongeze”Amesema Tabu Shaibu.

Amewataka Wananchi wote walopo Ndani ya Wilaya yake , Mkoa wa Dar es Salaam na nchi kwa ujumla wajenge utaratibu wa kushirikiana na Viongozi wao kutatua kero ndogo ndogo ambazo zitaokoa kiasi cha pesa ambacho kitaweza kutumika kwa ajili ya mambo mengine.

Naye Diwani wa Kata ya Kisukuru, Mh : J oseph Saenda, amempongea Afisa Hbari huyo kwa kujitolea kufuatilia maslagambo huo aliouitisha  na Wananchi na kusema wataendelea na utaratibu huo kwa kuwa imeshakuwa ni utamaduni wao.

Amesema kipande cha bara bara hiyo, kinasababisha magari mengi kuharibika haswa ikinyesha mvua jambo ambalo linaathiri uchumi wa watu wengine na kata kiujuma kwani katika kata hiyo kipo Kiwana cha Nafaka hivyo kama magari hayata pita uzalishaji utapungua.

“ Hii ni bara bara kubwa sana, inatumika na magari yote iiwamo Segerea, Tabata, External na Segerea, hivyo tumeona tuchukue hatua maana mvua
ikinyesha haipitiki na inakuwa ni hatari kwa wanafuzni wetu kukosa usalama “Amesema Diwani Saenda

Aidha amesema katika uwasilishaji wa marekibisho ya bara bara hiyo walishapeleka maombi manispaa wao wakichangia mafuta lakini majibu ni kwamba Greda hilo lilikuwa Gareji kwa ajili ya Matengenezo licha ya bara bara hiyo kuwemo katika mpango wa TARURA.

Naye Mwanchi wa Kata hiyo, Nelson Dugo, amempongeza iwani huyo kwa ubunifu wake wa kutatua kero ndongo ndogo katika kata yake huku akisema mwamko mkubwa umetokana na wananchi hao kupokea taarifa hiyo ya diwani wao kwa mikono miwili ili kuletaa maendeleo.

AAkihitimisha zoezi hilo, Afisa Hbari, Tabu Shaibu, amewataka wananchi kujitolea katika shughuli za kjamii kwani maendeleo hayana chama na wale wenye kutaka kuweka siasa katika maendeleo waachane na dhana hiyo kwani Rais Magufuli anataka watanzania na watu wote wafanye kazi.

Post a Comment

emo-but-icon

item