DC Mjema aitaka TAKUKURU kuchunguza Taasisi ya Wamachinga Kariakoo

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/10/dc-mjema-aitaka-takukuru-kuchunguza.html
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, ameitaka TAKUKURU kuchunguza shutuma za Wamachinga dhidi ya Viongozi wa Taasisi hiyo.
Hayo ameyasema Leo wakati akiendelea na ziara yake ya Kata ya 36 katika Jimbo La Ilala. Akizungumza na Waandishi wa Habari, DC Mjema, amesema kitendo cha watu kuuza Mali ya Umma ni kinyume na Sheria na Utaratibu.
Amesema amekuwa akipatiwa tuhuma hizo na malalamiko mengi Ofisini kuhusu Wafanya Biashara hao kutoridhishwa na utendaji wa Viongozi katika Mtaa Taasisi yao .
Aidha, amesema wapo baadhi ya watu wachache wamejitengenezea mazoea ya kuuza maeneo yaliyopo pembezoni Mwa bara bara wengine wanauza kuanzia Milioni moja na nusu hadi laki 8 kwa kila kipande cha eneo.
Amesema Serikali ya awamu ya tano, haijatoa hayo maelekezo ya watu kuuza maeneo Bali iliamua kuwa tambua rasmi na kutaka kila mtu afanye kazi.
Hata hivyo, amesema maamuzi yake ya kuanzisha Taasisi hiyo yakikuwa na lengo la kuwakutanisha wafanya Biashara moja kwa moja na kuwaweka Utaratibu mzuri, lakini cha kushangaza bado watu wachache wanaojinufaisha wenyewe kwa kujali maslahi yao binafsi kuliko ya Taasisi.
" Mlitaka nisema Sasa achaniseme kwamba tuliwapatia uhuru na utaratibu wa kufanya kazi lakini mnageika Sasa namuagiza Afisa TAKUKURU wakishirikiana na Afisa Utumishi Manispaa ya Ilala pitieni hizi tuhuma zote kwa taratibu zenu na kama kuna watu wanacheza rafu hizo awatie ndani na kufunguliwa kesi Mahakamani"Amesema DC Mjema.
Katika kujibu tuhuma za uuzwaji wa meza, DC Mjema, amemuagiza Afisa Masoko Manispaa ya Ilala kukutana na wafanya Biashara hao kwa ajili ya kuratibu utaratibu mpya wa ugawaji wa Meza.
Amesema hadi kufikia Tarehe 27 mwezi Oktoba 26 utaratibu wa meza utakuwa umekamilika.
Naye Mfanya Biashara ndogo ndogo ( Machinga), Iddy Omary , ameilalamikia Ofisi ya Wamachinga huku akidai ofisi hiyo ina ukiritimba na hawaja na maamuzi ya kupata wa Mkandarasi wa meza.
Amewataka Viongozi wote wanaongoza Taasisi hiyo ikiwamo Mwenyekiti wa Taasisi ya wafanya Biashara, Lusinde kuachia ngazi ikiwezekana wawa chague wakina mama kwakuwa wanaweza.
Katika hatua nyingine wafanya Biashara hao kwa nyakati tofauti tofauti, pamoja na shutuma Za Meza , wamekuwa wakitolewa matusi, kejeli na vitisho na Uongozi wa Taasisi hiyo ya KAWASSO .
DC Mjema amesema Serikali ya awamu ya tano inataka kila mtu afanye kazi, hivyo amemtaka Afisa Masoko kuhakikisha Taasisi hiyo inafanya mkutano mkuu kwa ajili ya kupanga upya utaratibu Katika utendaji wao.
Mbali na kukutana na wafanya Biashara wa Kariakoo, pia amekutana na wafanya Biashara wa Soko la Mchikichini Karume nakuwaambia ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mchoro wa Soko lao utakuwa umekamilika.
Amesema baada ya ujenzi wa Soko la Kisutu kumalizika litakalofuata litakuwa Karume. Hivyo amewaomba wale wanaohitaji hifadhi ya kudumu baada ya ujenzi huo wajisajiri waweze kutambulika. .
Pia DC Mjema amepokea kero kutoka Kata ya Gerezani zikiwamo ukosefu wa maeneo ambao ulipekea kuwa na ofisi 2 za Serikali za Mitaa.
Hard Rock Hotel & Casino Las Vegas, NV - Mapyro
ReplyDeleteA 동두천 출장마사지 map showing Hard 광명 출장안마 Rock Hotel & Casino 태백 출장샵 Las Vegas, NV, with road conditions 광명 출장안마 and free valet parking, Hard Rock Hotel 고양 출장마사지 & Casino Las Vegas