Naibu TAMISEMI, Josephat Kandege afurahishwa na uwazi wa miradi inayoendelea katika wilaya ya Temeke.


Naibu wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(TAMISEMI) Josephat Kandege afurahishwa na uwazi wa miradi inayoendelea katika wilaya ya Temeke.

Mh: Kandege amefanya ziara katika Wilaya ya Temeke ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya miradi ya maendeleo katika Mkoani Dar Es Salaam, 
Miradi hiyo ambayo imefadhiliwa na Banki kuu ya Dunia.

Lengo kuu ya ziara yake ni kujiridhisha na utekelezwaji wa miradi hiyo na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati. Pia kukagua usalama wa wananchi wanaoishi karibu na ujenzi wa miradi hiyo. 

Hata hivyo amerizishwa na utendekaji kazi na kasi ya miradi hiyo inavyoendelea. Ameipongeza ofisi ya Mkurugenzi kwa jinsi inavyosimamia vizuri mapato na matumizi ya fedha za miradi.

Miradi ambayo imetembelewa ni pamoja na ujenzi wa jengo la ofisi ya DMDP lilipo katika eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,ambalo lilmekamilika na kutumika.


Barabara ya Mwanamtoti, Daraja la kijichi Toangoma,Soko na Stand ya kijichi ambayo yote imefikia katika hatua nzuri. Miradi yote hii inatarajiwa kukamilika kufikia mwezi wa pili mwakani.

Related

habari 4252621446892263326

Post a Comment

emo-but-icon

item