Mtarawanje aanza kuyavaa majukumu ya Udiwani Kijichi leo

https://raiatanzania.blogspot.com/2017/12/mtalawanje-aanza-kuyavaa-majukumu-ya.html
DIWANI mpya wa kata ya Kijichi, Mh: Eliasa Kassim Mtarawanje, leo ameapishwa rasmi kushika madaraka ambayo yaliachwa na mtangulizi wake aliyekuwa diwani Mamam Tausi Milazni ambaye alifariki dunia mwaka huu.
Tukio la kuapishwa kwa Diwani huyo mpya, limefanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Manispaa na kuhudhuriwa na Baraza la Madiwani la Manispaa, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke na wakuu wa idara na vitengo.
Mtarawanje, ambaye alitangazwa kuwa mshindi na Mkurugenzi wa Manispaaya Temeke katika uchaguzi uliofanyika Nov 27, nakujipatia ushindi huo kwa kura 2658 kupitia chama cha CCM, ameapishwa mapema leo na mwanasheria wa Halmashauri ya Temeke.
Uchaguzi huo ulifanyika baada ya kufariki madiwani wawili kwa mda tofauti katika kata hiyo.