Mburahati All Stars Veterani yapoteza mchezo dhidi ya Vijana FC

TIMU ya Soka ya Mburahati All Stars Veterani, imepoteza mchezo wake dhidi ya Vijana FC mara baada ya kukubali kipigo cha Mabao 6-2 kwenye mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Uwanja wa Mpira uliopo Chama cha Soka cha Kinondoni.



Akizungumza mara baada ya mchezo kumalizika, Diwani wa Kata ya Makurumla , Omary Kijiko, amesema ilikuwa si mategemeo kupoteza mchezo huo kwani timu yao ilijipanga kuondoka na ushindi.
Image may contain: 1 person, standing, shoes, sky and outdoor
Aidha, Kijikio, amewapongeza wachezaji wenzake kwa jitihada walizo zionesha kwenye mchezo huo licha ya kupoteza huku pongezi kubwa akiitoa kwa Vijana FC kwa kuonesha kandanda safi 

"Nawapongeza sana Wachezaji wangu, tuliingia kwenye mchezo ili tushinde ila hatujafanikiwa, lakini Vijana wameonesha mchezo mzuri sana hivyo nawaomba wazidi kupambana kwani soka la sasa lina jengwa na Vijana ambao ndio watakuwa mkombozi wa kesho katika maendeleo ya Soka hapa nchini". Amesema Kijiko

Naye Mfungaji wa Kwa upande wa Timu ya Mburahati All Stars Veterani, Idd Mnenge maarufu kama Rio, amesema ilikuwa sio bahati kushinda kwani walipoteza nafasi nyingi za wazi ambazo  kama wengekuwa makini wangepindua matokeo

"Mchezo tuliuanza Vizuri sana, ila bahati haikuwa kwetu, ila sikitiko langu nilitamani kumaliza mchezo mpaka mwisho, majeruhi niliyopata yaliniradhimu kutoka nje, lakini tuna jipanga kesho (Jumapili ) tutakuwa na mchezo mwengine naamini tutafanya vema". Amesema Rio

Magoli ya Mburahati All Stars Veterani yaliweka kimyani na Nassoro Umbi na Idd Mnenge huku mabao ya Vijana FC yakifungwa na Razaro, Ayubu Piro (Yanga B), Ally Chuchya (2), Chandai (2).

Related

michezo 1577606810651969591

Post a Comment

emo-but-icon

item