Jiji la Dar es Salaam lapata tuzo kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.

https://raiatanzania.blogspot.com/2017/12/jiji-la-dar-es-salaam-lapata-tuzo.html
JIJI la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017 kati ya majiji 90 ambayo yameshiriki mashindano kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.
![]() |
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies .
![]() |
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka, lengo ikiwa kuangalia majiji ambayo yamefanya vizur katika Sekta ya Miundombinu ambapo kwa upande Dar es Salaam tunzo hiyo imepokelewa na Mstaiki Meya wa jiji hilo Isaya Mwita.
![]() |
Picha ya tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies iliyotolewa kwa jiji la Dar es Salaam Chicago Nchini Marekani.
Baadhi ya majiji ambayo yamepata Tuzo hizo ni Dar es Salaam, New York pamoja na Cap Town ambapo kwa upande wa Jiji la Dar es Salaam imewakilishwa na Mstaiki Meya Mwita,aliondoka nchini Disemba 3 kuelekea nchini Marekani ambako mashindano hayo yalifanyika Disemba 5 na kurejea nchini Tanzania Disemba 8 mwaka huu .
![]() |
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine huko Chicago Nchini Marekani wakiwa wameshika tuzo zao. |
Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya mafanikio ya tuzo jijini hapa.
Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi Duniani.