DC Mjema, Naibu Meya Ilala kutajirisha Jogging za Dar es Salaam




Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema pamoja na Naibu Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto, leo wame sherekea sherehe ya kutimiza miaka miwili ya Tramp Jogging ya Vingunguti huku wakiahidi neeema lukikuki juu ya Vyama hivyo.

Jogging ya Tramp  iliyoanzishwa Agosti 12 mwaka 2014, ni miongoni mwa Jogging zinazofanya vizuri Wilaya ya Ilala, kwani mpaka sasa wamejikita katika ujasiriamali kama vile kutengeneza mito pamoja na kumiliki boda boda moja inayowaingizia kipato licha ya ukosefu wa wafadhili mbali na Kumbi lamoto kujitolea bado wanahitaji zaidi wafadhili wakutosha.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua uzinduzi huo, DC Mjema, amesema atahakikisha Jogging zote zinakuwa na mfuko maalumu wa kifedha ambao utasaidia kutatua changamoto zao ili kuondokana na utegemezi walio nao kwa sasa.
DC Mjema, amesema ni wakati wa Jogging kuamka na kuachana na dhana ya kufanya mazoezi pekee na kuangalia fursa nyingine za kiuchumi ambazo zitaweza kubadilisha maisha yao pamoja na kunyanyua pato la Taifa tunapoelekea Tanzania ya Viwanda kaulimbiu ambayo inasimamiwa na Rais Magufuli.


Aidha DC Mjema, amesema kama alivyopambana kufanikisha kila Jogging inakuwa na chama chake na katiba yake hivyo hivyo ndivyo atakavyo simamia maslahi ya wana Jogging kwa kutambua umuhimu wake katika Taifa na maendeleo kwa ujumla.


"Jogging zote kwa sasa zinatambulika Kitaifa kama ilivyo michezo mingine, nawaomba isitokee mtu akawatia doa, hatupo kisiasa na kama kuna watu wachache wanataka kuwaharibia kwa matendo yao mabaya watoeni mapema na kuwachukulia hatua,  kikubwa mzingatie sheria mnapokimbia mkaombe kibali mtapewa na mtafanya mazoezi yenu bila tatizo, pia naombeni majina matano ya kila Jogging ili kutoa fursa ,  kuna 5% ya Halmashauri inayotolewa kwa Vijana, nawaomba Viongozi wa Jogging zote Alhamis ya wiki hii mfike Ofisini kwangu kuwapatia elimu hiyo nakuona ni kwa namna gani itawasaidia kujiendeleza"Amesema DC Mjema

"Andaeni kiasi kidogo cha fedha ambapo ifikapo Februali 2, 2018 nitatengeneza harambee nita washirikisha rafiki zangu tuta andaa mahali ili zoezi hilo lifanyike lengo likiwa ni kutunisha mfuko wenu  wa fedha katika kuendesha shughuli zenu za kimaendeleo"Ameeongeza DC Mjema

Hata hivyo, DC Mjema amejibu risala yao huku akiwa ahidi  kuwatimizia kwani vitu walivyoomba vipo ndani ya uwezo wake huku akianza kuwapatia Kompyuta moja ya Ofisi akiahidi Boda boda kumpa muda ambapo atakutana na Naibu Meya Kumbilamoto kuona ni kwa jinsi  gani watafanikisha hilo suala.


Pia amewaahidi kuwatangazia Biashara zao za ujasiriamali wa kutengeneza mito kwa wadau wake ambao watakuwa wanunuzi wazuri wa bidhaa hiyo kitu ambacho kitawaongezea uzalishaji mali wa Jogging hiyo ili kuepukana na utegemezi
Katika upande wa miundombinu, DC Mjema, amewataka wamiliki wa vyombo vya moto wampe muda kwani atahakikisha Bara bara hiyo inayounganisha Vingunguti na Mnyamani inamwagwa Vifusi atakavyoviomba kutoka Tazara na Jengo la Tanesco Ubungo ili kusubilia ujenzi kamili kupitia Tarura.
Mbali na hayo, DC Mjema amempongeza Rais Magufuli kuwatoa wafungwa kwa kibali chake hususani Mwanamziki nguli hapa nchini mwenye urai wa Kongo, Nguza Viki maarufu kwa jina la Babu Seya  huku akiwaasa wana Jogging watii sheria kwani kukaa jera kuna nyima uhuru wa mtu.
Naye Naibu Meya wa Ilala, Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto, amempongeza DC Mjema huku akisema ndiye Mteule pekee aliyeteuliwa na Rais Magufuli anayefanya vizuri kwa kufuata maagizo ya Rais Magufuli katika kuharakisha maendeleo yanakua kwa kasi hususani Wilaya ya Ilala.
Kumbilamoto, amemuomba DC Mjema kushirikiana nae bega kwa bega kuonana na mama mfuko wa Jogging zote ili kuwajengea uwezo wa Jogging  zijitegemee  kiuchumi na kuwatoa kwenye dimbwi la umasikini.

"DC Mjema mimi kwangu namuona ni mwanamke wa shoka, mama jasiri anayepambana kuona watu anaowaongoza wanafikia malengo yao, tunamshukuru kuja hapa na kuacha majukumu yake mengine, kikubwa namuomba apokee risala yetu na kuifanyia kazi kama tunavyotarajia, alipambana kuhakikisha Jogging zinatambulika naimani kwa hili eltu hatotuangusha, vijana hawa wa leo ndio vijana ambao mwaka 2020 tunategemea ndio wataompeleka Dododma akiwa kama Mbunge wetu "Amesema Kumbi lamoto
Naibu Meya Kumbilamoto, amempongeza sana Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya zenye dhamira ya kweli ya kutaka kubadilisha muelekeo wa Taifa kuonekana kuwa na ramani nzuri kimataifa katika nyanja zote ikiwamo Siasa, Uchumi, Elimu, pamoja na maendeleo ya utamaduni na michezo.
Pia amechukua  nafasi ya kumpongeza zaidi baada ya kumtoa Babu Seya akidai yeye ni mmoja wa wadau wa msanii huyo aliyetokea kumteka sana na vibao vyake vyenye ujumbe maridhawa.


Katika uzinduzi huo, ulihudhuriwa na baadhi ya watendaji wa Serikali ikiwamo Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu, Kassimu Mshamu, wenye viti wastaafu wa mitaa mbali mbali kata ya Vingunguti pamoja na Mwenyekiti S/Mtaa wa Mtakuja, Sharifu Mbulu na msanii mkongwe aliyeimba zaidi ya miaka 8 makwi Zaire,Mafumu Bilali Bombenga.

 









Image result for hospitali ya vingunguti

Related

habari 5011776701963032690

Post a Comment

emo-but-icon

item