Uhamiaji yawashikila watu 16 wanaodhaniwa ni Wahamiaji haramu katika Ziara ya DC Mjema Kata ya Mchikichini










NAIBU Kamishina Afisa Uhamiaji Manispaa ya Ilala, Pili Zuberi, amewashikilia jumla ya watuhumiwa 16 wanaodhaniwa kuwa Wahamiaji haramuuwa  Katika ziara iliyofanyika Leo ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, kwenye kata ya Mchikichini.

 Tukio hilo limetokea Leo Mara baada ya mkazi mmoja  kutoa tuhuma za kuwepo kwa watu wasiojulika na kuhifadhiwa Mtaa wa Msimbazi Bondeni.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari , DC Mwema, amesema msako wa Vijana hao kukamatwa , ulianza mara baada ya kufuatia kero iliyotolewa na mkazi mmoja ya kutokuwa na imani nao.

DC Mjema amesema kama mtu  anataka kufanya kazi Tanzania lazima Sheria na utaratibu wa nchini ufuatwe.

 " Hii ni nchini huru, hakatazwi mtu  kujakufanya kazi, lakini lazima afuate utaratibu na Sheria, hivyo wale wote wanaokuja nchini wataje kazi wanazokuja kuzifanya pamoja na muda watakao tumia kuishi hapa " Amesema DC Mjema.

Aidha amesema kuwa kazi hizo wanazozifuata watanzania wanaziweza.

Hata hivyo, amempongoza OCD wa Wilaya ya Ilala pamoja na Naibu Kamishina Afisa uhamiaji Manispaa ya Ilala, Bibi Pili Zuberi kwa ushirikiano wao wa kukomesha kitendo cha uvamizi katika kuhakikisha Ilala inakuwa  salama.

Amewataka Wakazi wa Kata ya Mchikichini, kutoa ushirikiano ili kuweza kugundua wahamiaji haramu, vibaka pamoja na uharifu kwa ujumla.

Naye Naibu Kamishina Afisa uhamiaji Manispaa ya Ilala, Pili Zuberi  Mdanku, amesema kwa mujibu wa kazi lazima wapitie hatua za kazi kwa ajili ya kuwachukulia maelezo.

Amesema kama watagundua ni wahamiaji haramu watachukua hatua Kali za kisheria huku akiwataka wanaozamia nchini waache haraka tabia hiyo na kufuata utaratibu wa nchi.




.


.




Post a Comment

emo-but-icon

item