RC Makonda: Wafanya biashara Mwezi wa ramadhani sio wa kutafuta faida

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wafanyabiashara kuachana na dhana ya kutaka kujipatia faida kubwa kila inapofika Mfungo wa Ramadhani.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua mwenendo wa Ujenzi wa Ofisi za Waalimu, amesema mwezi huu ni mwezi wa toba ambapo mtu anataka kufanya jambo zuri la kumfurahisha Mwenyezi Mungu na sio mwezi wa kukamuana kiuchumi kama baadhi ya wafanya biashara walivyozoea.

RC Makonda amesema yupo tayari kuona kila mwananchi ndani ya mkoa wake ananufaika vizuri na bidhaa zilizopo kwa gharama nafuu kwani amejipanga kuhakikisha anaongeza muda wa wafanya biashara kufanya shughuli  zao hadi saa 6 usiku.

""Nitoe raia kwa wafanyabiashara, zingatieni faida ndogo msitake vikubwa lazima mtambue huu ni mwezi wa kuchuma swawabu na sio kumkandamiza mteja, mkifanya hivyo hata biashara zenu Mungu atazibariki, nami sitokuwa nyuma nitajitahidi kuendana na mwezi huu angalau nami nipate neema ya mwezi kwakuwa mfungo huu ni sehemu pekee ambayo neema inashuka, nataka kusema muabudu muda wote hakuna wakuwazuia ""amesema RC Makonda 
Amesema lengo la kuongeza muda ni kutaka kuona bidhaa zikiuzwa na wale waliopo kwenye mfungo wanapata fursa ya kununua vitu wavitakavyo na kutoa mwanya kwa waliokosa muda wa maandalizi wajue kwamba watapata huduma kama kawaida.
Image result for wafanyabishara kariakoo

Post a Comment

emo-but-icon

item