RC Makonda akutana na Wahanga wa Nyumba Mbagara, afunguka mazito

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh:Paul Makonda, amefunguka mazito hii leo ikiwa ni  baada ya kutembelea nyumba zilizobomolewa kufuatia na mvua kali iliyonyesha hivi karibuni katika Kata ya Kilungule, Wilaya ya Temeke.

Akizungumza na Waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo, RC Makonda, amesikitishwa na majanga hayo yaliyotokea huku akiwapa pole wale wote waliofikiwa na matatizo hayo, lakini hakusita kuwatolea uvivu wale wote waliojenga kwenye mabonda akisema kwamba tayari walishakatazwa na walishindwa kusimamia sheria pasipo kujua madhara yake baadae.

RC Makonda, amesema kuwa watu wanaokiuka sheria  na katazo la kujenga mabondeni wakati walishapatiwa utaratibu ndio wanaochangia  kwa kiasi kikubwa athari hizo kwani mwaka jana jumla ya Shilingi  Milioni 400 zilitumika kwa ajili ya kununulia dawa za kuulia wadudu wanaotamba kama vile Mbu, hivyo uzembe wa namna hiyo unajirudia kila siku tumechoka tunachowataka ni kuhama maeneo hayo na kutafuta mahala penye usalama zaidi.









1






Post a Comment

emo-but-icon

item