Picha ya Ozil, Gündogan na Erdogan yazusha hasira kubwa Ujerumani

Mesut Özil (kushoto) alimkabidhi rais Erdogan jezi yake ya ArsenalHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMesut Özil (kushoto) alimkabidhi rais Erdogan jezi yake ya Arsenal
Shirikisho la soka Ujerumani (DFB) limeshutumu wachezaji wake wa kimataifa Mesut Özil na Ilkay Gündogan kwa kupiga picha na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Wachezaji hao wawili waliozaliwa Ujerumabni, wote wenye asili ya Kituruki, walimkabidhi Erdogan fulana zao walizozisaini katika hafla moja mjini London siku ya Jumapili.
Gündogan aliandika: "kwa mtukufu rais wangu, kwa heshima kubwa." Erdogan anafanya kampeni ya kutaka kuchaguliwa upya kama rais Uturuki.
Özil anaichezea timu ya Arsenal na Gündogan anaichezea Manchester City.
Woote wawili wanajitayarisha kwa kombe la dunia mwezi ujao nchini Urusi, ambapo Ujerumani ni miongoni mwa timu zinaozpigiwa upatu ushinda. Uturuki haikufuzu.
Nyota watatu wa Uturuki walipiga picha na bwana Erdogan (kutoka kushoto): Ilkay Gündogan (Man City); Mesut Özil (Arsenal) na Cenk Tosun (Everton)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNyota watatu wa Uturuki walipiga picha na bwana Erdogan (kutoka kushoto): Ilkay Gündogan (Man City); Mesut Özil (Arsenal) na Cenk Tosun (Everton)
Wansiasa wengi Ujerumani wamewashutumu wachezaji hao wa soka, wakihoji uadilifu wao kwa maadili ya demokrasia ya Ujerumani.
Rais wa shirikisho hilo la soka Ujerumani DFB Reinhard Grindel amesema: "Soka na DFB zinalinda maadili ambayo hayaheshimiwa vya kutosha na Bwana Erdogan.
"Ndiyo sababu sio vizuri kwa wachezaji wetu wa kimataifa wakubali kuhadaiwa na kampeni yake ya uchaguzi. Kwa kufanya hivyo, wachezaji wetu hawajasaidia jitihada za DFB katika kushughulikia utangamano."
Mkurugenzi wa DFB Oliver Bierhoff amesema: "hakuna kati yao aliyetambuwa ujumbe unaotokana na picha hiyo, lakini ni wazi kwamba ni makosa na tuazungumza nao kuhusu hilo".
Katika ujana wake, kabla ya kuingia katika siasa katika miaka ya 90, Erdogan aliichezea timu ya Istanbul, Kasimpasa.
Erdogan, ambaye amehudumu kama kiongozi wa Uturuki kwa miaka 15 sasa anatafuta kuchaguliwa tena katika uchaguziw a dharura Juni 24.
Rais Erdogan na mkeweHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais Erdogan na mkewe
Baada ya shutuma hizo kuzuka, Gündogan ametoa taarifa akijitetea, pamoja na wachezaji Özil na Cenk Tosun kuhusu kukutana na Erdogan.
Walikutana kando kando mwa hafla moja kwenye taasisi ya Uturuki inayowasaidia wanafunzi wa Kituruki, alieleza.
"Je tunapaswa kuwa wajeuri kwa rais wa nyumbani wanakotoka familia zetu?" aliuliza.
"Kwa shutuma zozote zilizopo, sisi tuliamua kuonyesha ukarimu na upole kutokana na heshima kwa ofisi ya rais na kwa asili yetu ya Kituruki."
Alisema "sio nia yetu kutoa ujumbe wowote wa kisiasa kwa picha hii".

Related

michezo 7663998641063651852

Post a Comment

emo-but-icon

item