Mwanaharakati wa Saudi Arabia adai kupata vitisho
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/mwanaharakati-wa-saudi-arabia-adai.html
MARWAN NAAMANI/AFP/GETTY IMAGES
Mwanamke aliyejikita kwenye Kampeni kuhakikisha wanawake wanaruhusiwa kuendesha magari nchini Saudi Arabia anasema yeye na wenzake nchini humo wanatishiwa
Manal al-Sharif amesema amekuwa akipokea vitisho vya kukatishiwa uhai wake wakati huu wakisubiri marufuku hiyo kuondolewa rasmi.
Wanaharakati hao wamekuwa wakishutumiwa wakiitwa wasaliti na kuwa wanafanya kazi kwa maslahi ya nchi zenye nguvu duniani, shutuma ambazo shirika la Amnesty International linaona ni hazina msingi na ni mbinu za kutishia tu.
Kundi hilo linashutumiwa kuwasiliana na mashirika ya nje ili kudhoofisha uimara wa Saudi Arabia.
Manal al-Sharif, ambaye sasa anaishi nchini Australia, amesema Kampeni hii inayowalenga wanaharakati ni sawa na ile iliyokuwa ikipinga kampeni hizi mwaka 2011.
Marufuku inatarajiwa kuondolewa tarehe 24 mwezi Juni.
Watu saba, wanawake na wanaume walikamatwa mwanzoni mwa juma hili.Wanaaminika kuhusisha Loujain al-Hathloul, mwanaharakati mashuhuri kwenye kampeni za kutaka haki za kuendesha magari kwa wanawake.
Bi Hathloul alikamatwa awali, ikiwemo mara moja mwaka 2014 alipojaribu kuendesha gari katika eneo la mpaka kutoka jumuia ya nchi za kiarabu, alishikiliwa kwa siku 73.
JASON SCHMIDT
Amnesty inasema kuwa inaamini kuwa wanawake wanaharakati Eman al-Nafjan, Aziz al-Yousef, Dr Aisha al-Manea, Dr Ibrahim al-Modeimigh, and Mohammad al-Rabea wamekamatwa pia.
Sheria za Saudi Arabia zinawataka wanawake kupata ridhaa za wanaume kwenye maamuzi mbalimbali na utekelezaji, na hali hiyo ilifikia hatua ya kupiga marufuku wanawake kuendesha magari.
Awali, ilimaanisha kuwa familia zililazimika kuajiri madereva ili kuwasafirisha ndugu zao wa kike.
Mwanamfalme Mahammad Bin Salman ametambulika kama mtu wa 'Mabadiliko' lakini ahadi kama hizi zimegonga mwamba kutokana na kudhibitiwa kwa wanaharakati kama hao ambao wengi wao walio mstari wa mbele kwenye kampeni ya kuwepo na usawa wa kijinsia wako korokoroni.