Matope ya volkano yatishia kituo cha umeme Hawaii


Aerial view of lava fissure near power plantHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMatope ya volkano karibu na kituo cha umeme cha Puna
Matope kutoka mlima Kilauea huko Hawaii yameelekea kitua cha umeme, hali ambayo imewalazimisha wafanyakazi kuzima mitambo kwa hofu ya kuvuja gesi za sumu.
Wafanyakazi waliondoa bidhaa zinazoweza kushika moto kwa haraka na visima vya vyenye kina kirefu vya kituo hicho vimejazwa maji baridi na kufungwa
Ikiwa matope hayo ya volkano yataingia kwenye visima hivyo inaweza kuvuja gesi yenye sumu ya hydrogen sulphate
Matope yanayosonga kwa mwendo wa chini yaliingia eneo la kituo hicho Jumatatu na tangu wakati huo yamesimama.
LavaHaki miliki ya pichaUSGS
Image captionMatope ya moto yakirushwa kutoka kwa mlima
"Hauwezi kutabiri ni wapi yataelekea au ni lini yatafika huko," afisa wa huduma za dharura za Hawaii alisema,.
Maafisa wa kaunti walisema matope hayo yako umbali wa takriban mita 270 kutoka kisima kilicho karibu.
Bw Travis alisema mvuke unaweza kutoka, kemikali kadhaa na pia gesi ya hydrogen sulphide ambayo ni hatari sana.
Watoa huduma za dharura walihamisha ndoo 60,000 na gesi yenye kushika moto kutoka kituo hicho.
Lava fissure aerial viewHaki miliki ya pichaUSGS
Image captionMatoke yakisonga kusini mwa mlima Kilauea
Lava fountains out of a fissureHaki miliki ya pichaUSGS
Image captionMatope ya moto
Kituo hicho cha umeme huzalisha karibu asilimia 30 ya umeme unaohitajika kwenye kisiwa hicho kwa kutumia mvuke unaotoka chini ya ardhi.
Lava flows into the Pacific Ocean south-east of Pahoa during ongoing eruptions of the Kilauea volcano, HawaiiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMoshi kutoka kwa volkano
Mlima Kilauea ulilipuka mwanzo wa mwezi Mei na hali kwa wenyeji wa eneo hilo inazidi kuwa mbaya.
An aerial view of a massive flow of fast moving pahoehoe consuming everything in its path, as the flames from the remnants of one home burnHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMatope ya volkania yaliharibu nyumba

Post a Comment

emo-but-icon

item