DC Mjema akagua Mabanda ya Wajasiriamali waliojitokeza katika Maonesho Mnazi Mmoja leo

Mkuu  wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema  leo amekagua Mabanda mbali mbali ya Wajasiriamali waliojitokeza kuonyesha bidhaa zao katika maonesho ya Wajasiriamali yaliyoandaliwa na Manispaa ya Ilala yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.


 Akizungumza na waandsihi wa habari leo kwenye viwanja hivyo, DC Mjema, amesema kuwa lengo la kuwajumuisha Wajasiriamali hao ni kutangaza biashara zao.


DC Mjema amesema  maonesho hayo ni bure , kwani yatatoa mwanga wa kuona ni kwa jinsi gani mikopo waliyoitoa imezaa matunda kwa wajasiriamali hao katika kipindi cha miaka mitatu.
 

"Halmashauri ya Manisipaa ya Ilala imekuwa ikitekeleza majukumu yake katika kuwaibua, kuwawezesha, kuwaelimisha na kuwaendeleza  wajasiriamali wadogo wa kati na wakubwa kupitia mpango bajeti kwa kuzingatia Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM"amesema DC Mjema 
Mjema amesema  manispaa ya Ilala ilitenga siku  nne za maonyesho ya biashara wajasiriamali mbalimbali waliopo Ilala ili kutangaza bidhaa zao , ambapo yalianza Alhamisi ya tarehe 16 ya mwezi huu na kilele chake kinatarajiwa kufanyika kesho tarehe 19, 2018.

Aidha katika maonesho hayo tumeshuhudia tuzo mbali mbali zikitolewa kwa mabanda bora ya biashara ambayo yameonyesha ushindani katika maonyesho hayo kwa mwaka huu 2018.

Amesema  Ilala ina takriban wajasiriamali 15,000  ambao wapo katika vikundi v
ikubwa na vidogo wenye shughuli za pamoja na mmoja mmoja    .

Mjema amesema katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2014 ,2015,2017 hadi 2018 Ilala imekuwa ikitenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ili kuwawezesha wajasiriamali hao katika mfuko wa kujiendeleza wanawake na vijana.

"Katika mpango

huu wa kusaidia vijana jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimekopeshwa kwa vikundi vya wanawake na vijana 2,978  ambapo kati yao vijana 8,482 na wanawake 6,906  walinufaika "Amesema .

Akielezea changamoto katika jitihada mbalimbali  za kusaidia vikundi amesema  wajasiriamali wengi hasa wadogo hushindwa kunufaika na mfumo huo kutokana na masharti mbalimbali.

Mjema amesema  kutokana na changamoto hizo wamezingatia maelekezo serikali ya awamu ya tano kupitia viongozi mbalimbali na kufanya maboresho ya mfumo huo ili kukidhi mahitaji ya wajasiriamali.

Post a Comment

emo-but-icon

item