Mwenyekiti kamati ya maadili ya shina la JPM ataka mshikamano dhdi ya Wamachinga
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/03/mwenyekiti-kamati-ya-maadili-ya-shina.html
MWENYEKITI wa kamati ya maadili ya Shina la CCM JPM lililopo Kariakoo Mtaa wa
Kongo na Mchikichi, Omary Irunga, amewataka wana CCM wawe na umoja na
mshikamano katika kuelekea uzinduzi wa shina hilo unaotarajiwa kufanyia hivi
karibuni.

Akizungumza na Raia Tanzania, Omary, amesema ni
wakati wa kuungana na kushirikiana kwani mshikamano ndio chanzo cha kujenga
fursa nzuri ndani ya chama na kuleta matokeo chanya ya kimaendeleo.
Aidha, Mwenyekiti huyo
amewataka wajumbe wanaoinda shina hilo waondokana na unafiki maana kama
watakuwa na unafiki utaharibu mshikamano wao na kuleta picha mbaya miongoni mwa
wananchama wao na kuiletea sifa mbaya Chama cha Mapinduzi CCM.
Amesema ni wakati wajumbe
kushirikishana kwa kila jambo ili kufikia maendeleo na kuachana na majungu
yasiyo na maana.
"Mshikamano muhimu
sana, lakini mshikamano wetu utajengwa kama maadili yatazingatiwa ipasavyo,
hatuwezi kufikia maendeleo kama tunasimamia majungu, unafiki na fitina,
tukumbuke mwamvuli tuliojifichia umebeba roho za watu wenye imani na sisi, wanahitaji kuona wanafikia maendeleo ,
hivyo ni wakati wetu sasa kuacha kukumbatia dhambi ya uoga na badala yetu
tuseme ukweli ambao utamkomboa Mmachinga katika kufikia Tanzania ya Viwanda na
Uchumi wa kati"Amesema Omary
Katika hatua nyingine,
Mwenyekiti wa Shina, Hamisi Sadiki, amewataka wajumbe wote waliojiandikisha
katika shina hilo waende kuonana na Uongozi ili wajiandikishe upya na walipie
kadi zao kwani muda uliobakia ni mdogo.
Naye mjumbe wa Shina hilo,
Kaisi Nassoro, amesema kuwa ili kufikia maendeleo katika shina hilo ni lazima
kila kiongozi ajitambue na ajue majukumu yake na kwa wananchama wake bila
kupepesa macho na kuyumbishwa kwani CCM ya sasa tofautin na ya zamani .
Katibu wa Shina, Anani
Helah, amewataka wajumbe wote waliokata tamaa na uzinduzi wa shina hilo wawe na
amani kwamba taratibu za uzinduzi zinafuatwa na wakati wowote mambo yatakuwa hadharani.


