Mr. Nice afunguka bifu na Young Dee

https://raiatanzania.blogspot.com/2017/12/mr-nice-afunguka-bifu-na-young-dee.html
MSANII aliyetamba hapa nchini na kibao cha Kikulacho,Mr. Nice amefunguka mazito huku akitishia kumchukulia hatua kali msanii mwenzake wa Bongo Flava Young Dee.
Mr. Nice, alimtuhumu Young Dee kwa kitendo cha kutumia miondoko na
mashairi ya wimbo King’asti katika ngoma
iliyotambulika kwa jina la kiben.
Hayo alizungumza Kupitia radio Swahiba FM 102.9 ya Zanzibari,
kwenye kipindi cha burudani cha Power Beat , ambapo Mr. Nice alifunguka kuwa Young Dee hamfahamu wala kumtambua Young
Dee.
“Hili suala sio jema sisi kama wasanii kuchukuliana
milio sio vizuri, kuna utaratibu, kama angefuata utaratibu tusingefikia huku
tunapotaka kwenda lazima tubadilike haki ya mtu haiuzwi”. Alisema Mr. Nice
Kutokana na tuhuma hizo, Mr. Nice, alipanga kumchukulia
hatua kali kwasababu ya kuiba wimbo wake wa king’asti.