Huyu ndiye beki tishio kwa Kichuya Vpl

https://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/huyu-ndiye-beki-tishio-kwa-kichuya-vpl.html
Winga hatari wa Klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania Shiza Ramadhan Kichuya amemtaja beki ambaye huwa anamhofia zaidi kila wanapokutana kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara VPL.
Shiza ambaye amekuwa na Sifa ya kusumbua mabeki wengi kila anapocheza pembeni ya uwanja kutokana na Kuwa mjanjmjanja awepo uwanjani lakini pia naye wapo mabeki anaowahofia wanapokutana.
Shiza amemtaja Paul Ngalema ambaye kwasasa yupo Lipuli ya Iringa kuwa ndiye beki tishio kwake awapo uwanjani kutokana na Aina ya Uchezaji wake, Akizungumza kwenye kipindi cha Soka Kijiweni cha Azam Tv amesema
Yule sasahivi yupo Lipuli alikuwa Ndanda namba 3 Paul Ngalema, Yule bwana akisema leo ntamtoa nje unaweza ukatoka kama ukiwa mpumbavu, kwanza akija ujiandae kwanza angalia mwili wake halafu unamuona akija kwenye mwili kama wa kwangu halafu ndo kaamua.
Paul Ngalema amecheza timu mbalimbali Ligi kuu ikiwemo Simba, Ndanda ila kwasasa anakipiga katika klabu ya Lipuli timu ambayo itakutana na Simba Jumapili Hii katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam. Kuzipata Exclusive za Kimichezo kila siku like Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini.